Nape Nnauye amesema kuwa baada ya yeye kuwa mbunge mwezi mmoja au miwili baadae zilianza kusambazwa picha za wanafunzi wakiwa wanasoma chini ya darasa hilo ambalo hali yake ilikuwa mbaya kwani lilikuwa ni darasa la miti tu huku wanafunzi wakikaa kwenye miti pia.
"Nikiri kwamba msukumo wa ile picha kwenye mtandao wa jamii ulikuwa na mguso wa pekee yake kuliko ningesimuliwa kawaida, baada ya kuona ile picha imesambaa na anayesemwa ni mimi nikaaamua kufunga safari nikaja nikasema jamanii hii ni aibu kwetu tumesemwa kwamba vijana wetu wanasoma kwenye darasa bovu kwa hiyo nikaamua na kukaa pamoja na wenzangu tukaweka mkakati.
"Nikaleta mifuko ya cement na kuanza kazi ya kufyatua tofali tukaanza na madarasa machache hivyo tulipigana kutoka kwenye hili darasa kwenda kwenye hayo madarasa mengine ambayo sasa yamefika manne na tunaendelea kwani tunataka iwe shule yenye madarasa ya kutosha na ikiwezekana na nyumba za walimu" alisema Nape Nnauye