Polisi Wafunguka Kuhusu Tukio la Afisa Ubalozi wa Syria Kushambuliwa

Polisi Wafunguka Kuhusu Tukio la Afisa Ubalozi wa Syria Kushambuliwa
Leo March 21, 2018 Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Jumanne Murilo amezungumza na waandishi wa habari katika ofisi zake kuhusu kushambuliwa kwa Afisa wa ubalozi wa Syria nchini H. Alfaori na kuibiwa Euro 93,000 sawa na Shilingi Milioni 251 za Kita March 20, 2018.

“Tukio la unyanganyi kwa kutumia nondo lililofanyika kwa mhasibu wa ubalozi wa Syria, akiwa anatoka kwenye ubalozi huo akiwa na dereva ambae tunamtafuta, dereva huyo aliacha kupita njia ya kuelekea mjini huku akiendesha gari polepole sana,” -RPC KINONDONI

“Mhasibu alivamiwa na watu watatu ambao wanatuhumiwa kuwa ni majambazi, walimjeruhi kwa kipande cha nondo kichwani, wahalifu wakaondoka na dereva pamoja na gari ya ubalozi,” -RPC KINONDONI
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad