Prof. Jay Awasii Watanzania Kuwezesha Soko la Musiki

Prof. Jay Awasii Watanzania Kuwezesha Soko la Musiki
Rapa mkongwe ambaye pia ni Mbunge Joseph Haule 'Prof. Jay' amewasii mashabiki wa muziki nchini kurejesha utamaduni wao wa kununua albumu za wasanii ili kuwezesha soka la muziki kuwa bora zaidi ya zaidi na kutoa ajira kupitia sanaa wanayoifanya.


Prof. Jay ametoa kauli hiyo mchana wa leo (Machi 17, 2018) kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii baada ya kuwepo kwa imani kwa baadhi ya wasanii wakiamini kwamba albamu za muziki haziwezi kuwalipa kutokana na mashabiki zao kuzoea tamaduni ya ku-donwload wimbo bure huku wengine wakiwasubiri wachache wanunue kisha wao waombe watumiwe kwa njia ya simu.

"Ninaamini sana ni haki ya msingi sana ya mashabiki wa muziki kupata albamu kutoka kwa wasanii wanaowapenda na kuwa-support lakini pia albumu ni kipimo kizuri sana kwa msanii kuweza kujua mashabiki wake wanataka nini au wanaipokeaje sanaa yake na anatakiwa aongeze au kupunguza kitu gani ili kufikisha ujumbe wake kwa hadhira aliyoilenga", amesema Prof. Jay.

Aidha, Prof. Jay amesema licha ya yeye kuamini kuwa kuongeza kwa soko la albamu kuna muweka msanii kwenye kumbukumbu isiyoweza kufutika kirahisi lakini wanapaswa wafahamu kwamba albamu ni kama kitabu na nyimbo zinakuwa kama 'chapters' hivyo inaweza kudumu miaka na miaka.

"Kipekee naomba sana nitoe wito kwa mashabiki wote wa muziki Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kurudisha tena ule utamaduni wa kununua albumu za wasanii wetu ili kuliweka soko la muziki wetu kuwa bora zaidi kuliko ilivyokuwa hapo zamani ili tuweze kupata ajira nyingi zaidi kupitia sanaa yetu, Kwani wakati ni sasa", amesisitiza Prof. Jay.

Mpaka sasa wasanii wachache waliweza kuachia albumu kupeleka kwa mashabiki zao huku wengine wakiwa njiani kufanya hivyo ili kuweza kujiwekea historia ya maisha yao katika kazi ya sanaa ambayo wanafanya kwa kizazi cha baadae.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad