Profesa Jay ajitokeza na kuwapa neno Basata


Msanii mkongwe wa muziki wa hip hop na Mbunge wa Mikumi, Profesa Jay, amefunguka juu ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kufungia wasanii na baadhi ya kazi zao, na kusema kuwa suala hilo sio sahihi.

Jay amesema BASATA wanapaswa kukaa na wasanii na kuzungumza nao, ikiwezekana kutoa semina elekezi, lakini sio kuwafungia kwani wasanii wanapitia mengi magumu kwenye kutengeneza kazi zao.

“Unajua asilimia kubwa ya taifa ni vijana, na wengi wao wanajishughulisha na sanaa mbali mbali, suala la kufungiwa huu muziki tumetoka nao mbali sana, mtoto akikosea usimchinje kichwa, tujaribu kufanya semina elekezi, kumfungia mtu kama roma ni kitu kikubwa, hii inarudisha nyuma na inakatisa tamaa”, Professor Jay alikiambia kipindi cha EATV.

Prof Jay ameendelea kwa kusema kwamba yeye kama muwakilishi wa wananchi na wasanii pia, atalisemea hili bila kuchoka.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad