Taarifa kutoka nchini Sudan Kusini ni kwamba Mamlaka ya Vyombo vya Habari nchini humo jana March 9, 2018 imefunga radio inayomilikiwa na Umoja wa Mataifa.
Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, radio hiyo iitwayo Radio Miraya imefungwa kutokana na kushindwa kufuata masharti na sheria za vyombo vya habari nchini humo.
Inaelezwa kuwa chombo hicho cha habari kimekuwa kikipokea vitisho vya kusitishiwa shughuli zake na mamlaka hiyo tangu mwaka 2016 na hatimaye jambo hilo limefanyika.
Akizungumzia suala hilo mbele ya vyombo vya habari, Mkuu wa Mamlaka hiyo Elijah Alier Kuai, ameeleza kuwa radio hiyo imeshindwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria zinazoongoza vyombo vya habari na hiyo ndio sababu kubwa ya kufungiwa.
‘Kuna kikundi kimetumia mtandao wa Telegram kuhamasisha maandamano’-Polisi Makao Makuu