Rais Xi Jinpingwa China Achaguliwa Kuwa Rais wa Maisha

Rais Xi Jinpingwa China  Achaguliwa Kuwa Rais wa Maisha

Rais Xi Jinping ateuliwa rasmi kwa rais bila ukomo wa mihula ya kuongoza. Bunge la nchi hiyo pia limemteua Xi ally Wang Qishan kuwa Makamu wa Rais

Rais Xi mwenye umri wa miaka 64 anatajwa kuwa kiongozi mwenye ushawishi mkubwa zaidi baada ya alieyekuwa kiongozi wa kihistoria wa nchi hiyo Mao Zedong

Bunge lilipiga kura kupitisha marekebisho ya Katiba na kuondoa ukomo wa rais kukaa madarakani. Rais wa sasa Xi Jinping aruhusiwa kutawala bila kikomo.

Katika mchakato huo ulihusisha Wabunge takribani 3000 waliopiga kura na wakati wa kutolewa kwa matokeo ni Wabunge wawili tu ndio walipiga kura ya hapana dhidi ya mabadiliko hayo
Katiba ya China ilikuwa ikitoa uhalali kwa Rais kukaa madarakani kwa muda usiozidi vipindi viwili tu huku kila muhula ukiwa hauzidi miaka 5(kama ilivyo kwa Katiba ya Tanzania)
Mwezi uliopita chama cha Kikomunisti cha China kinachoongoza taifa hilo kilitoa pendekezo la kuondolewa kwa ukomo wa mihula ya Rais na Makamu wa Rais na leo wamehitimisha kwa kupiga kura
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad