RC Dodoma Ampa Mkandarasi Wiki Mbili

RC Dodoma Ampa Mkandarasi Wiki Mbili
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge ametoa muda wa wiki mbili kukamilishwa kwa mkandarasi wa mradi wa Umwagiliaji unaofadhiliwa na Mpango wa Chakula Duniani WFP, ambao ulitarajiwa kukamilika mwaka 2017 wilayani Chamwino.


Maelekezo hayo ameyatoa katika ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya Kilimo inayotekelezwa wilayani Chamwino itakayogharimu zaidi ya shilingi milioni 800 ambapo vijiji vitatu vinatarajia kunufaika na mradi huo.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema kwa muda uliobaki mkandarasi huyo hana budi kupelekea mafundi wote katika eneo la mradi ili kuukamilisha kwa wakati licha ya changamot zilizokuwepo hapo awali.

"Jitahidini kuanzia leo mtakuwa mmebakisha wiki mbili tu. Yaani piga ua nataka mradi ukamilike haraka iwezekanavyo. Wewe tafuta hata mafundi wako msiangalie kwamba mtapata nini sidianeni,  mafundi washirikiane na Injinia huu mradi ukamilike," Mahenge.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad