RC Makonda Atoa Kauli Nzito kwa Waliotoa Waraka wa Kuikosoa Serikali

RC Makonda Atoa Kauli Nzito kwa Waliotoa Waraka wa Kuikosoa Serikali
Ni vigumu sana Kusimama Katika HAKI Kwenye Dunia iliyojaa Uovu , Kwamaana Unapigwa Katika Kila Upande  na Hata Waliotakiwa Kuzama Katika Maombi nao Wamekengeuka .

Ninapoitazama Kazi ya Msalaba Naelewa Kwanini Yesu Kristo alibaki Peke Yake .

Umepigana VITA ya Madini sikuona Waraka , Umejenga Ukuta Mkubwa Mererani Kulinda Rasilimali Yetu ya Tanzanite , Sikuona Waraka ,Umepigana Vita ya Rushwa,Umeanzisha Mahakama za Mafisadi sikuona Waraka Umepambana na Wazembe Maofisini sikuona Waraka, Umetoa Elimu BURE Sikuona Waraka , Umefufua Shirika la NDEGE, Unajenga  Treni ya Mwendo Kasi (SGR) Sikuona Waraka. Umeanzisha Mchakato wa Ujenzi wa Vyanzo Vipya Vya Umeme (Stigglers Gorge), Hatujaona Waraka.

Lakini Kama Haitoshi Umekomesha Mauaji ya Kutisha Ya Rai wasiokuwa Na Hatia kule Kibiti , Hatujaona Waraka ,Umekomesha Tabia Ya Askari kuvamiwa Na kuuwawa Vituoni wakiwa wanatimiza  Majukumu yao Ya Kulinda Raia , Hatujaona Waraka.Nakumbuka Kulikuwa na Tabia Ya kutorosha Wanyama kwa Kuwapandisha Ndege, Leo Umekomesha , Hatujaona Waraka .

Lakini Niwakumbushe , Umeongeza Bajeti ya Ununuzi wa Madawa Na Vifaa Tiba Kutoka Bilioni 31 Mpaka kufika Bilioni 260 , sijawai Kuona Waraka .

Tangu Umeingia Madaraka Umeongeza Vivuko katika Maeneo Yote Yanayohitaji Vivuko vya Majini , pamoja Na Madaraja Ya Kupitia Juu kwa wananchi Kuvuka , Pamoja Na Ununuzi wa Meli Kubwa Za Mizigo Na kubeba Abiria, Sijaona Waraka.

Umeamisha Makao Makuu ya Nchi Kupeleka Dodoma ,Unaongeza Uzalishaji wa Umeme Huku Ukiwapelekea Wananchi Mpaka Vijijini , Umeongeza Nidhamu Serikalini Unaongeza AJIRA Kupitia Viwanda , Yote haya na Mengine Mengi  Sijaona Waraka .

Leo Hii wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam Wanaunganishiwa Maji Mpaka kwa Mkopo , Sijaona Waraka.

Leo Hii Mtulia Kuhama Chama Ambapo Ni Haki yake Kikatiba Ndio Nimeona Waraka .Ninakusihi na Kukuomba nikiwa  Mtumishi wa Mungu Ninae TAMKA  mambo na Kutokea.

Ninaye Yaona Mambo Yasiyo ONEKANA kwa  macho ya Mwili, Naiona Tanzania Mpya katika Uongozi wako.Shupavu.
Usifadhaike wala usihuzunike  kwa Sababu Unayoyasikia LEO na Kuyaona Hutayasikia tena kwa jina la Yesu Krsito Mwana wa Mungu aliye Hai.

Nakwasababu Wamebadili Kusudi la Kufa kwa Yesu Kristo , na kupoteza maana ya Pasaka.Bwana wa Majeshi anakwenda Kupindua Meza zao Kama ilivyotokea YERUSALEM.. Endelea.

Ujumbe huu Ukawatie Moyo Watu Wote Wanaoipenda Nchi na Kukuombea   kwa Roho na KWELI

 Ni mimi Mtumishi Wenu
 Paul Makonda
 Niliyepewa kipande cha Dar es salaam

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Usalama wa raia na mali zao ni bora kuliko umeme na maji.

    Haki, usawa, na uhuru- ni bora kuliko SGR na Madini

    Amani, utulivu, na ustawi wa wananchi - ni bora kuliko kuongeza vivuko na madawa.

    Amani kwanza, Uhuru kwanza, utulivu kwanza, usawa kwanza, na ustawi wa nchi kwanza. Mengine yatakuja kama ziada.

    ReplyDelete
  2. Watanzania ni watu wa hovyo. Like father like son. Ikiwa hao Maaskofu hawajitambui na kujua nini wajibu wao hasa katika jamii vipi raia wa kawaida? Makonda yupo sawa kabisa na anasema kwa vitendo. Maaskofu wamethibitisha ni watu wa kutumika na ndio waliotumika kuwawekea mazingira mazuri Wakoloni wakati wanakuja kuitawala Afrika. Na ndio waliochochea vurugu za Rwanda hadi kufikia kuchinjana kama kuku. Kutokuwajibika kwa watumishi kiroho kikamilifu katika mambo yanayowahusu na kutumika kisiasa ndiko kunako pelekea kuongezeka kwa vitendo viovu, ukimwi nakadhalika.

    ReplyDelete
  3. well said...HAKIKA WANATUMIKA....

    HATA KAULI KWAMBA WALIFUNGA....HAITEGEMEWI KUTOKA KWA KIONGOZI MKUBWA WA DINI KUFUNGA NI SIRI...HUWEZI KUTAKA KUHARARISHA JAMBO ETI TU KWASABABU UMEFUNGA.....JE WAKATI NCHI NZIMA HAINA MADAWATI WALIFUNGA ILI MUNGU ALEGEZE MIOYO YA WATU WASAIDIE HILO??


    UKWELI UKO HIVI...HAKUNA ANAYEFANYA JAMBO JEMA KABISA AMBALO NI LA KIMUNGU ANAKUBALIKA ....WENGI WETU TULIKUWA TUMELOWEA KWENYE KILA AINA YA UKIUKAJI WA SHERIA NA MAADILI LEO HII MTU ANAKUJA KUTURUDISHA HAKIKA HATAPENDWA HAKIKA HAKIKA HATAPENDWA....

    BY THE WAY

    SHETANI ANACHUKIA MEMA NA ANA-PROMOTE MAOVU ....TUWENI WAANGALIFU...HAOGOPI HATA KUMTUMIA KIONGOZI WA DINI SEMBUSE NA LEO HII AMBAO BABA ZETU WAKIROHO KAZI ZA KIROHO ZIMEKUWA NI SECONDARY????

    MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU BARIKI MAMLAKA ZILIZOPO KWANI HAKIKA HAKUNA MAMLAKA AMBAYO HUJIWEKA NYENYEWE....

    ASANTE KWA KUTUPATIA KIONGOZI ANAYETURUDISHA SI TU KATIKA MSTARI WA KUTIMIZA WAJIBU ZETU KAMA RAIA HAPA DUNIANI LAKINI ANATUSAIDIA PIA TUACHANE NA MATENDO AMBAYO NI DHAMBI NA CHUKIZO KWAKO MUUMBA WETU..

    ReplyDelete
  4. Hivi hao maaskofu ndio wale walorudisha ule mgao wa ESCROW?? Inauma-iyoooo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad