Msanii wa Hip Hop Roma Mkatoliki ni miongoni mwa mastaa waliotajwa na Naibu Waziri wa sanaa, Utamaduni na Michezo Juliana Shonza kufungiwa kwa nyimbo zao na kupewa onyo kali ila kwa upande wa Roma alifungiwa miezi sita.
Lakini Leo March 21,2018 nakusogezea mambo matano aliyoyazungumza Roma Mkatoliki katika interview aliyofanya na XXL ya Clouds Fm.
…….>>>“Mwaka jana nilipata ujumbe kutoka BASATA na ulikuja kwa njia ya sms kuhusu wimbo wa Kibamia nikaitikia wito uliyotolewa ila utata ulikuwepo kwenye ujumbe uliyopo kwenye wimbo huo”
….>>>”Nilipokea tamko la kufungiwa katika muziki ila wakati muda haujaisha mke wangu alikuwa anakaribia kujifungua na mambo mengine mengi”
….>>>”Nimeshangazwa kufungiwa kutokana na wimbo wa Kibamia na wimbo huo umejadiliwa kama wimbo wa Roma pekee wakati ni wa kundi la ROSTAM”
…..>>>”Mimi, Madee na Askofu tulienda ofisini kumuona Naibu Waziri wenzangu walimuona lakini mimi sikufanikiwa wenzangu waliitwa pekee yao, mimi nikaambiwa sina ruhusa ya kwenda kuingia ndani, ningefanyaje?”
….>>>”Hapo kati kulikuwa na upepo mzuri wa ROSTAM kwahiyo tulikuwa tushalipwa pesa kwaajili ya show nyingi za miezi ijayo sasa hivi tunapigiwa simu turudishe pesa za watu lakini pia nimefanya jitihada kutafuta viongozi wa BASATA na Wizara ili kupata muafaka wa jambo hili lakini bado sijafanikiwa”