March 9, 2018 kimefanyika kikao cha bodi ya barabara {ROAD BOARD} mkoa wa Kagera, ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa uliopo manispaa ya Bukoba, ambapo imeibuka changamoto ambayo halmashauri inakumbana nayo juu ya Kampuni ya ujenzi MECCO.
Meya wa manispaa ya Bukoba Chief Kalumna amesema walipokea fedha za mradi wa barabara kutoka benki ya Dunia takribani Billion 6 na walitangaza zabuni ya ujenzi wa barabara hizo, kampuni ya ujenzi Mecco ilishinda katika mchakato huo lakini wameitwa kusaini mkataba wamekataa bila sababu zozote hali iliyopelekea manispaa kushindwa kutekeleza mradi kwa muda uliopangwa na kuamua kutangaza zabuni upya.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa Kagera Meja Jeneral mstaafu Salum Kijuu amemuagiza Mkuu wa polisi Kagera kumkamata mkandarasi huyo na kumfikisha ofisini kwake akiwa na pingu ili aweze kueleza kwa nini amesababisha usumbufu huo.