Said Kubenea Alipuka Ataka Tume Huru ya Uchaguzi Bungeni

Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea amesema amepeleka bungeni barua ya kusudio la kuwasilisha hoja binafsi ya kuwa na chombo huru cha kusimamia uchaguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Machi 11,2018 Kubenea amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) si chombo huru cha kusimamia uchaguzi.

Amesema barua hiyo aliiwasilisha Alhamisi Machi 8,2018 katika ofisi ya Katibu wa Bunge mjini Dodoma, Kubenea amesema uchaguzi kusimamiwa na Tume isiyo huru inaweza kusababisha machafuko.

"Hatuwezi kuacha hali hii iendelee, vurugu zimekuwa zikitokea kwa sababu ya kuwa na Tume ya aina hii, tunataka chombo huru," amesema.

Amesema tangu nchi iingie katika mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 uchaguzi umekuwa ukifanyika kwa kusimamiwa na Tume isiyo huru.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad