Serikali Yaiomba Benk ya Dunia Kukopeshwa Dola Milioni 150

Serikali Yaiomba Benk ya Dunia Kukopeshwa Dola Milioni 150
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango ameiomba Benki ya Dunia (WB), kuipa Tanzania mkopo wa Dola 150 milioni za Marekani ili kuchochea ukuaji wa uchumi na utoaji wa huduma nchini.

Dk Mpango ametoa ombi hilo alipokutana na Mkurugenzi wa Uchumi Mpana, Biashara na Uwekezaji wa Benki ya Dunia, Felipe Jaramilo katika ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango jijini DSM ambapo Waziri Mpango alifanikiwa kumuelezea Mkurugenzi huyo namna Uchumi wa Tanzania unavokua.
Waziri Mpango ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kuisaidia Serikali ya Tanzania haswa hii iliyopo madarakani katika kutekeleza miradi ya maedeleo nchini.

“Pamoja na ukuaji mzuri wa uchumi, Taifa bado linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo ukosefu wa ajira kwa vijana, kiwango cha umasikini bado kiko juu, ukuaji mdogo wa sekta ya kilimo na kupungua kwa mikopo ya benki za biashara kwa sekta binafsi,” Dk Mpango.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad