Serikali Yatoa Kauli Hii Kuhusu Waraka wa Maaskofu

Serikali Yatoa Kauli Hii Kuhusu Waraka wa Maaskofu
Waraka uliotolewa na Baraza la maaskofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri chini Tanzania (KKKT) mwishoni mwa wiki iliyopita umeendelea kuibua mjadala mkubwa nchini.

Katika waraka wa ujumbe wa pasaka, baraza hilo limeorodhesha mambo kadhaa ambayo wameyataja kuwa ndio tishio la umoja na amani ya nchi.
Mambo hayo kwa mujibu wa waraka huo ni Utekwaji wa watu ,utesaji, kupotea kwa watu, mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi, vitisho, ubambikiziaji wa kesi, na matumizi mabaya ya vyombo vya dola.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, alipoulizwa msimamo wa serikali kuhusu waraka na matamko mbalimbali ya viongozi wa dini  alijibu kuwa   kwa sasa serikali haioni cha kujibu na kwamba inawatakia tu waumini kheri ya Pasaka.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad