Serikali Yawachagulia Wananchi Kifo


Serikali ya nchini Austria jana ilipiga kura kupinga katazo la kutouzwa na kuvuta sigara kwenye migahawa na baa nchini humo ambalo lilikuwa limewekwa na serikali iliyopita ya nchi hiyo, hii ikimaanisha sigara zitauzwa na kuvutwa kama kawaida maeneo hayo.

Utekelezwaji wa jambo hili utaanza rasmi mwezi May mwaka huu. Wabunge wameeleza kuwa jambo hilo linalenga kulinda ‘uhuru wa kuchagua’ wa wananchi wa Austria huku pia ikilinda maslahi ya wenye biashara ya migahawa na bar.

Hata hivyo mwanasiasa mmoja ameeleza kuwa uamuzi huo wa serikali ni kama kufanya maamuzi ya kuwachagulia kifo wananchi wa nchi hiyo. Inaelezwa kuwa jumla ya watu 13,000 wanakufa nchini humo kwa matatizo ya afya yanayotokana na uvutaji sigara.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad