Shaffih Dauda baada ya Yanga kupoteza mechi ya kimataifa nyumbani

Kumekuwa na maoni mengi na mitazamo tofauti baada ya mechi ya Caf Champions League kati ya Yanga dhidi ya Township Rollers mchezo ambao umeshuhudia yanga ikipoteza nyumbani kwenye uwanja wa taifa kwa kufungwa 2-0 ikiwa ni mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza.

Wengi wao wametoa maoni kwa kuangalia matokeo ya uwanjani kwa upande wa Shaffih Dauda pia ametoa maoni yake kwa kueleza sababu kadhaa za Yanga kupoteza mechi hiyo lakini amegusia mambo mengi ikiwemo ubora wa ligi, maandalizi pamoja na vitu vingine

Wakati mwingine matokeo kama haya yanatupa mtazamo mpana wa kuangalia mambo mengine ambayo sisi tunayafanya na kuridhika nayo kutokana na mazingira ya kwetu na tunaona tupo sawa labda kutokana na mazoea.

Kwenye mechi kama hizi ili uweze kufanya vyema, ni lazima yawepo maandalizi yanayotokana na mamo mengi, kuna maandalizi ya makocha na benchi la ufundi kufanya kazi yao ya kumtambua mpinzani wanaekutana naye, hilo ni jambo la kwanza lakini wawe wanapata support kutokana na mfumo wa ligi yao na nchi yao kwa ujumla.

Yaani mpango wa maendeleo ya mpira kitaifa katika nchi yao, mamlaka husika wametekeleza majukumu yao kwa kiasi gani? Ukija kwenye ligi yao ‘Botswana’ inaendeshwa kwa utaratibu upi? Level ya ushindani kwenye ligi yao ipoje? Performance na viwango vya wachezaji kutoka katika timu tofautitofauti upoje?

Vitu vyote hivyo ni matokeo ya wadau wengi kwa maana ya vilabu vyenyewe vinamajukumu yake kuhakikisha wanaandaa mifumo mizurikutengeneza klabu zao, mamlaka zingine kwa mfano zinazosimamia ligi jukumu lao ni kuhakikisha ligi inakuwa ya ushindani ambayo itatoa bingwa ambaye atakwenda kushindana na mabingwa kutoka kwenye mataifa mengine na akawawakilishe vyema kuonesha ni namna gani ligi yao ilivyo bora na kwenda kuitangaza. Sasa kwetu, vitu vyote hivyo huwa hatuvipi kipaumbele huwa ‘tunajifanyiafanyia’.

Kilichobadilisha matokeo kwenye mechi ya Yanga na Township Rollers ni level ya performance, wenzetu level yao ilikuwa juu ukilingabisha na performance ya Yanga, Yanga walikuwa kama asilimia 50 ukilinganisha na wale Township Rollers kuanzia mchezaji mmojammoja kuja kwenye timu nzima. Naona baadhi ya watu wanazungumzia mchezaji mmojammoja kama vile Kessy, Tshishimbi, Chirwa, Yondani, lakini timu ndiyo inakupa matokeo.

Kwa mfano Kessy anafahamika kwa style yake ya uchezaji, ni ‘wing back’ anayekimbia pembeni, lakini ili upate kilicho bora kutoka kwake lazima apate ‘connection’ ya wenzake ambao wapo maeneo mengine watekeleze majukumu yao ili yeye anapokimbia na kupiga pasi ndani na anapokimbia kwenye mstari wa pembeni akutane na mpira kwenye nafasi aweze kupiga pasi ya mwisho wakati huo mshambuliaji awe amefika eneo la kufunga.

Wale Township Rollers kuanzia kwenye eneo lao la ulinzi walikuwa bora na walikuwa wanajua nawafanya kitu gani na ili waweze kutekeleza mipango aliyoizungumzia mwalimu, jambo la kwanza ni lazima wawe fit. Level ya fitness ya wachezaji wa Yanga unaweza kuiona iko chini ukilinganisha na wachezaji wa Rollers hata ukiangalia walivyokuwa wakigombea mipira ‘one against one’ walikuwa wanafanikiwa zaidi kuliko wachezaji wa Yanga. Walipokuwa wana mpira kwenye himaya zao hakuna mchezaji wa Yanga aliyekuwana uwezo wa kuuchukua.

Ukiangalia goli la pili, issue sio pasi kwa sababu unaweza ukapiga pasi hata 100 lakini upo kwenye eneo lako ambalo halimpi presha mpinzani ‘less pressure area’ mpinzani wako atakuwa anakuangalia tu unavyojifurahisha lakini unapovuka kwenda kwenye eneo la mpinzani ukiwa uanaendelea kupiga pasi maana yake wapinzani watatakiwa kuwa fit kwa kiasi kikubwa kwa sababu watatakiwa kukimbia sana kuziba ma-gape na kukaba ili kuuchukua mpira na nyinyi mcheze kwenda kwao.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tanzania masuala ya michezo sio mpira tu bali michezo yote hatupo serious kabisa. Mchezo wa mpira umesavaivi mpaka hivi sasa kwa kuwepokuwepo tu kwa kuwa unamapenzi na umejaa katika mioyo ya watanzania la sivyo ungelikwishasahulika na kupotea kama michezo mengine kama vile riadha na kadhalika. Hakuna jitihada za dhati na za kiyansi za kufufua michezo nchini kuendana na kasi ya mabadiliko na thamani ya michezo duniani kwa hivi sasa,bado tunaichukulia michezo kama mchezo na sio moja ya kati ya kicheceo muhimu kabisa cha maendeleo nchini. Sioni wizara husika kwa kipindi kirefu Tanzania ikiichukulia michezo kama moja ya jukumu lao kubwa kabisa kama sio namba moja kuhakikisha kuwa kuna maendeleo ya dhati ya michezo nchini itakayoliletea taifa faida. Dunia hii ya leo michezo ina faida sana tena sana kwa maendeleo ya nchi hasa kwa nchi kama Tanzania ambapo tumejaaliwa vivutio vingi vya kitalii lakini hakika gharama ya kuitangaza nchi yetu na vivutio hivyo vya kitalii ni kubwa mpaka tufikie kujijengea jina Duniani kwani biashara ya utalii inaushindani mkubwa duniani. Kuna nchi duniani hazina vivutio vya maana kama sisi lakini zinapesa na zinajua kabisa nchi kama Tanzania na vivutio vyake vya kitalii asilia vya maana ikiwa expose duniani itakuwa balaa kwani watakosa biashara,utakuta kuna nchi zimejenga mbuga bandia za wanyama na kuzipa mbuga hizo bandia majina ya mbuga zetu na kutokana na nguvu zao za pesa kuzitangaza mbuga hizo bandia zinapokea watalii wengi zaidi kuliko sisi. Kwa hivyo wanalolifanya ni kutumia nguvu kubwa za pesa walizonazo kununua watalii sisi hatuwezi kushindana nao. Tungekuwa genius enough kuitanagaza nchi yetu kwa kupitia vijana walioandaliwa vizuri kwenda kupeperusha Bendera ya Taifa kimataifa ingekuwa rahisi na effective kujitangaza. Lakini licha ya kulitangaza taifa kupitia michezo kikubwa zaidi ni kutengeza ajira kwa vijana nakadhalika nakadhalika. Kwa mfano sioni sababu mpaka leo vifaa vya Simba vya michezo kwa ajili ya kujiboreshea miundo mbinu yake izuiliwe na serikali kwa zaidi ya miaka mitatu sijui minne haingii akilini, leo Simba wanahangaika sehemu ya kufanyia mazoezi halafu tutarajie timu zetu kufanya vizuri kwa kweli ni kama vile mzee anamfanyia hujuma mwanae wa kumzaa ambae atakuja mfaa baadae. Simba kama walikuwa hawana uwezo wa kuzikomboa nyasi zao ungefanyika muafaka kati ya simba na wizara husika japo kuwakopesha kwa masharti sio kuzizuia zile nyasi bandarini mpaka leo wakati nnahakika hata hayo MAKINIKIA ya mchanga yaliruhusiwa kaondoka.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad