Shamsa Ford Atoa ya Moyoni Kuhusu Bongo Movie

Shamsa Ford Atoa ya Moyoni Kuhusu Bongo Movie
Leo March 8, 2018 Muigizaji wa Bongo Movie Shamsa Ford ameeleza ya moyoni baada ya maneno ya watu kudai kuwa Bongo Movie imekufa kutokana na zile kazi za zamani kutoonekana tena mtaani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram amewaomba directors kurudisha Bong movie kwenye soko kwani ndio msingi mkubwa  wa kuwapatia kipato na kutekeleza majukumu katika  familia hata kama wengine hawalioni hilo.



“Nilipoangalia hii tamthilia (bwana samlati )kiukweli nililia mpaka kwikwi utasema ni kweli kikubwa nilichogundua ni kwamba story, director na uchezaji ni vitu muhimu vya kuzingatia..ila sisi daaa sijui tutafika lini  huku    @jb_jerusalemfilms @richiemtambalike @raythegreatest@joharichagulatz @cloud112_mina_new@mrutu_lion @ johnlister fanyeni kitu jamani nyie ndo wenye bongo movie pls irudisheni.”

“kupitia nyie imetusaidia wengine kupata ajira na kuendesha familia zetu. sasa hivi bongomovie ilipo naumia kwasababu Mimi ni mmoja ambae ninaishi kutokana na kazi yangu si kama wale wanaosema hawaishi kwa kutegemea movie..Nawategemea wakubwa wangu pls”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad