Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Faiza Ally amefunguka kuwa wakati anakua hakuwahi kuwaza kuja kuwa ‘single mother’.
Faiza ameendelea kufunguka kuwa baada ya kuwa mama akawa anajiuliza
ni kwasasababu ya wanaume ndio aishi maisha asiyoyataka? alihoji.
Faiza kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika hivi “Wakati
nakua sikuwahi kuwaza kuwa single mom, lkn kutokana na misimimo yangu
wanaume wajinga hawakunielewa nikajikita ktk kujitegemea, baada kuwa
mama nikawa najiuliza ni kwa sababu tu ya mwanaume au baba mtoto ndio
niishi maisha nisiyo yataka , nikaondoka nikiwa nauchungu mwingi mno lkn
nikasema maisha yangu ni bora kuliko kuwa mke! Nikapitia mengi sana
haikua rahisi lkn
Leo nimesimama imara kwa sababu niliamua kuchagua
maisha ninayo ishi kwa hiari ! Nilipita wapi na nikavuka vikwazo vyote
????? Njoo nita share stori yangu na wewe kuwa single mom sio mwisho
wako ! Kuna maisha zaidi ya kukaa usipo stahili ! JUA THAMANI YA UANAMKE
WAKO BILA KUJALI WANAO BWEKA NJIANI“.