Silaha Iliyomgusa Akwilina Haijajulikana – Kamanda Mambosasa

Silaha Iliyomgusa Akwilina Haijajulikana – Kamanda Mambosasa
Kamanda Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amesema askari polisi waliotuhumiwa kifo cha Mwanafunzi wa chuo cha NIT, Akwina Akwiline bado uchunguzi unaendelea na haijajulikana ni silaha ipi iliyomgusa.



Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda Mambosasa amesema kuwa kama walivyotoa taarifa kutuhumiwa kwao na hata upelelezi utakapo kamilika wataeleza.

“Askari waliokuwa wametuhumiwa kuhusu kifo cha Akwilina ikumbukwe kwamba walivyokamatwa tulieleze bayana kwamba upelelezi unafanyika ili kujua ni nani ambaye ametenda kosa lile. Kwahiyo bado suala la upepelezi unaendelea yapo maelekezo ambayo yaliyotolewa.Ikumbukwe silaha moja ambayo haijajulikana ni ipi ndiyo iliyokwenda ikamgusa Akwilina lakini askari wale kama mnavyojua walikuwa ni wengi lakini pia kulikuwa hakuna ushahidi ni yupi alikuwa ametenda kwahiyo upepelezi bado unaendelea,“ amesema Mambosasa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad