Simba 200 Huuawa Kila Mwaka na Binadamu Tanzania


Habari ambayo iliripotiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC ni kwamba zaidi ya simba 200 huuawa kila mwaka nchini na wafugaji katika maeneo ya pembezoni mwa mbuga za wanyama na maeneo mengine ya uhifadhi.

Mtafiti na Mhifadhi kutoka Taasisi ya Utafiti ya Wanyamapori Tanzania Dr. Dennis Ikanda ameeleza kuwa kutokana na idadi ndogo ya simba duniani kuna umuhimu mkubwa kulinda rasilimali hii ili isiendelee kuharibiwa.

Dr. Ikanda ameeleza kuwa sababu kubwa ya kuuawa kwa wanyama hao ni ongezeko la mifugo ambayo huwafanya wafugaji kuhamahama ili kutafuta malisho kwa ajili ya mifugo yao hususani kando kando ya maeneo ya uhifadhi.

“Hii hufanya simba kukamata mifugo hiyo na wafugaji katika kutetea mifugo yao dhidi ya kuliwa na simba huwa huwaua.” – Dr. Dennis Ikanda
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad