Tafsiri sahihi ya kosa la uhaini na adhabu yake Kwa Mujibu wa Katiba ya Tanzania

Uhaini  ni  kosa  la  jinai, kwa tafsiri nyepesi ina maana kwamba ni kosa kubwa ambalo mtu analifanya dhidi ya nchi yake na mtu anyefanya kosa hili anajulikana kama msaliti, mfano wa watu wasaliti wanaojulikana duniani ni Yuda ambaye kidini alimsaliti Yesu, mwingine ni Benedict Anold huyu jamaa aliisaliti nchi yake ya Marekani dhidi ya Mbritishi, wengine ni Vidkun Quisling, na Marshall Pe’tain.

Kisheria ukubwa wa kosa hupimwa kwa adhabu yake, kosa likiwa kubwa mtuhumiwa hutumikia adhabu kubwa vivyo hivyo kosa likiwa dogo mtuhumiwa huadhibiwa kiasi.

Kwa mujibu wa sheria ya Tanzania, mtu akifanya yafuatayo huhesabiwa kama amefanya kosa la jinai la uhaini hivyo huadhibiwa kulingana na ukubwa wa kosa hilo.

Kifungu cha 39 ( 1 ) cha kanuni za adhabu kinasema kuwa mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri  ya Muungano au popote, kujaribu kumuua Rais, kuanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano,  kusababisha, kuwezesha, kuchochea, kushawishi, kushauri kuhusu  kifo, kumlemaza, kumzuia, kufungwa kwa Rais, kumwondolea Rais heshima na jina la mkuu wa nchi, amiri jeshi mkuu, au kiongozi wa serikali, kupindua serikiali iliyo madarakani, kutishia serikali, bunge au mahakama kwa makosa haya na yale yaliyotajwa hapo juu mtu wa namna hiyo atakuwa  ametenda kosa la jinai ambalo ni kosa la uhaini

Aidha ifahamike kuwa kwa mtu yeyote atakayekutwa na hatia ya kutenda kosa la uhaini adhabu yake ni kifo na sheria hiyo ya kifo imeelezwa katika kifungu cha sheria namba 39 na 40 cha kanuni za adhabu.

Hivyo watanzania kwa umoja wetu tunapaswa kuzijua sheria za nchi yetu ili kuweza kujiepusha kutenda makosa ya uhaini  dhidi ya nchi yetu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad