TRA yawasimamisha kazi watumishi wawili

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewasimamisha kazi watumishi wake wawili mkoani Lindi, kwa kile kilichodaiwa kwenda kinyume na kanuni na miongozo ya kazi inavyowaelekeza na kutumia lugha isiyo rafiki na wateja wao {wafanyabiashara}.

Uamuzi huo,umechukuliwa na Kamishina kodi ya Mapato za ndani nchini, Elijah Mwandumbya, wakati wa kikao cha pamoja kati yake na wafanyabiashara wa mkoa huo,kilichofanyika Manispaa ya Lindi baada ya kusikiliza malalamiko mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara hao.

Mwandumbya amesema Taifa wamekuwa wakipata taarifa kwamba hakuna mahusiano mazuri kati watumishi hao na wafanyabiashara, hali iliyohustua uongozi na kumtuma Kamishina huyo kufika mkoani humo kupata maelezo ya kina.

Kamishina huyo wa kodi za ndani amesema {TRA}  inapitia kipindi ambacho kinahitaji kuwapatia huduma bora wateja wao ili waweze kumsaidia Rais wa nchi katika utekelezaji wake wa maendeleo kwa kuhakikisha wanazingatia Sheria, kanuni, taratibu na miongozo,kuhakikisha wanatoa huduma iliyo bora kwa walipa kodi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad