Rais wa Marekani, Donald Trump ameamua kuweka wazi kuwa amechoshwa na kauli za vitisho kutoka kwa aliyewahi kuwa makamu wa Rais nchini humo wakati wa utawala wa Barack Obama, Joe Biden.
Trump amesema amechoshwa na kauli za vitisho juu yake zinazotolewa na mwanasiasa huyo mkongwe nchini Marekani kutoka chama cha Democratic na kuweka wazi kuwa haogopi chochote kwani anamjua toka enzi ni mtu asiyekuwa na nguvu kimwili na kiakili.
“Mpuuzi Joe Biden anajifanya kama mtu mwenye nguvu. Ukweli ni kwamba ni mtu dhaifu kimwili na kiakili mbaya zaidi anatishia kunipiga kwa mara ya pili hii. Nadhani hanijui vizuri nitamsambaratisha mara moja na kurudi nyumbani akilia njia nzima. Usipende kutishia watu.“ameandika Trump kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Jumanne Machi 20, 2018 Joe Biden akiongea na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Masuala ya siasa cha Miami akisema kuwa kama wangekuwa wanasoma naye sekondari angemchakaza kwa masumbwi Rais Donald Trump.
“Wananiuliza ninauwezo wa kufanya mdaharo na Trump, nawajibu hapana. Natamani kama tungekuwa sekondari ningempeleka kwenye eneo la kufanyia mazoezi nimchakaze kwa makonde mazito. Haiwezekani Rais wa nchi awachezee wanawake kwa kuwatomasa halafu aje aombe radhi hadharani heti alifanya makosa, hapa chama cha Republican kilichemsha,“amesema Joe Buddeni kwenye video hiyo iliyowekwa kwenye mtandao wa facebook wa chuo hicho.
Joe Biden anatajwa kuwa ndiye atakayekuwa mgombea wa urais mwaka 2020 kupitia tiketi ya chama cha Democratic na atashindana na Rais Trump kama atapita kwenye kura za maoni kwenye uchaguzi huo.