Tundu Lissu Kufanyiwa Upasuaji Mwingine

 Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mwingine wa goti la kulia Machi 14, 2018 katika Hospitali ya Chuo kikuu cha Leuven, Gasthuisberg ili kumnusuru asipatikane na athari za mifupa kutojiunga kwa wakati.

Lissu amebainisha hayo usiku wa kuamkia leo wakati alivyokuwa anawafahamisha umma juu ya maendeleo ya afya yanavyoendelea huko alipo na kusema anaendelea vizuri na matibabu na sasa anaweza kusimama kwa miguu yote miwili bila ya msaada wa magongo ya kutembelea.

"Timu ya madaktari bingwa wa mifupa wanaonitibu, wamenitaarifu kwamba kasi ya mfupa wa juu ya goti kuunga ni ndogo sana na  kwamba wasipoingilia kati na kurekebisha mfupa huo, itachukua muda mrefu sana kuunga na hata ukiunga baada ya huo muda mrefu, hautaunga kwa namna itakayoondoa hatari ya kuvunjika siku za mbeleni. Kwa sababu hizi, madaktari wangu wamependekeza kufanya operesheni nyingine kwenye mfupa wa juu ya goti la kulia", amesema Lissu.

Pamoja na hayo, Lissu ameendelea kwa kusema "Niko kwenye mikono salama ya kitabibu. Madaktari wangu, Prof. Dr. Stefa Nijs na Prof. Dr. Willem-Jan Mertsemakers, ni madaktari bingwa wa mifupa wanaosifika barani Ulaya kwa utaalamu wao katika fani hiyo. Hivyo msiwe na hofu, Mungu wetu aliyeniwezesha kuwa hai sasa, ataendelea kutenda miujiza yake kupitia kwa madaktari bingwa hawa. Nitaendelea kuwataarifu maendeleo ya matibabu yangu kadri itakavyokuwa lazima na muhimu kufanya hivyo".

Mbunge Tundu Lissu alishambuliwa na watu wasiojulikana tangu Septemba 7,2017 akiwa mkoani Dodoma, na kisha kupelekwa nchini Nai
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad