DAR: Ugonjwa wa Dengue umerejea nchini baada ya wagonjwa 11 kugundulika katika Hospitali ya Ocean Road
Wizara ya Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto imeeleza kuwa homa ya ugonjwa huo imendulika baada ya wagonjwa kadhaa waliokuwa na dalili zake kupimwa na kuthibitishwa
Mara ya kwanza ugonjwa huo uligundulika mwaka 2014 ambapo wagonjwa 400 waliupata. Walitibiwa na kupona, isipokuwa watatu ndiyo walifariki dunia
Tahadhari imetolewa kwa wananchi kupima afya haraka wanapohisi wana homa Kali, mafua na kuumwa kichwa kwa muda, ambazo ni dalili kubwa za homa ya dengue
Vimelea vya ugonjwa wa homa ya dengue husambazwa na mbu kama ilivyo kwa malaria. Hivyo wananchi wanahimizwa kuua mazalia ya wadudu hao haraka