Upande wa Utetezi Wataka Kitilia na Wenzake Wafutiwe Mashtaka ya Utakatishaji Fedha

Leo March 2, 2018 nakusogezea stori ya Kimahakama ambapo Upande wa utetezi katika kesi inayomkabili Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya, na wenzake umeutaka upande wa mashtaashtaka ya utakatishaji fedha ili washtakiwa wapate dhamana.

Mbali na Kitilya washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa miss Tanzania (1996), Shose Sinare na Ofisa wa benk ya Stanbic Sioi Solomon.

Wakili wa serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba kesi iahirishwe hadi tarehe nyingine.

Pia amedai kuwa mashtaka yanayo wakabili washtakiwa hayana kikomo na kwamba bado wanafanya juhudi za kuharakisha huo upelelezi.

Hata hivyo, wakili wa utetezi Majura Magafu amedai kama upande wa mashtaka haujakamilisha upelelezi basi liwe ahirisho la mwisho na pia wayafute mashtaka ya utakatishaji fedha ili washtakiwa wapate dhamana.

“Upelelezi umekuwa ndio wimbo wa kila siku takribani miezi 6 sasa, pendekezo letu kama upelelezi bado basi mashtaka ya utakatishaji fedha dhidi ya wateja wetu yaondolewe kusudi wapate sifa ya kudhaminiwa,” Wakili Magafu.

Baada ya kutolewa kwa hoja hizo, Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi March 16,2018 Kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa wanakabiliwa na makosa ya utakatishaji fedha, kwa kuhamisha, kuchukua na kuweka kiasi cha Dola za Marekani Milion 6 katika akaunti tofauti tofauti  za benki ambapo inadaiwa walitenda makosa hayo kati ya March 2013 na September 2015.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad