Upasuaji mkubwa wa mguu wa Tundu Lissu uliofanyika Brussels, Ubelgiji, umefanikiwa.
Taarifa kutoka katika hospitali alimofanyika upasuaji huo, zinaeleza kuwa madaktari wamefanikiwa kurekebisha mguu wa Lissu kwa mafanikio makubwa.
Huu ni upasuaji wa 19 kufanyiwa Lissu baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa mjini Dodoma, Septemba, mwaka jana.
Lissu ambaye ni mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), yuko Brussels kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa akiendelea na matibabu, akitokea Nairobi, Kenya alikokaa kwa zaidi ya miezi minne akitibiwa.