Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov amefahamisha kuwa ubalozi mdogo wa Marekani mjini Saint-Petersburg umefungwa na kufukuzwa wanadiplomasia 60.
Hatua hiyo imechukuliwa na Urusi kama jibu kwa Marekani na Magharibi na washirika wao kuhusu sumu aliopewa jasusi wa zamani wa Urusi Skripal.
Uingereza imewafukuza wanadiplomasia 23 wa Urusi na wengine 150 katika mataifa 25 ya mataifa ya Ulaya. Waziri wa mambo ya nje wa Urusi amesema kuwa uamuzi huo umechukuliwa kama jibu kwa huatua zilizochukuliwa mataifa ya Magharibi dhidi ya Urudi.