Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewapa siku 14 wafanyabiashara na wawekezaji walipo mkoani humo wawe wamemeshajiandikisha katika zoezi la vitambulisho vya taifa kwa wale ambao hawana mpaka sasa hivi.
Gambo ametoa kauli hiyo akiwa ofisini kwake kwa lengo la kuwapa vipaumbele watu hao kushirikishi katika zoezi hilo ili wasike kupata shida endapo watahitaji kuenda kuchukua hati ya kusafiri ambayo kwa sasa mpaka upatiwe ni lazima uwe na kitambulisho cha Taifa.
"Serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli ni serikali ambayo inajali makundi yote ya kijamii pamoja na wafanyabiashara. Tumeona ni muhimu kutengeneza utaratibu kupitia ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha kwa ajili ya kuwatengenezea mazingira rahisi wafanyabiashara na wawekezaji na kupitia mpango huo tumeona tuweke utaratibu maalumu wa kutenga wiki mbili kuanzia Marchi 15, 2018 ili waweze kushiriki kikamilifu", amesema Gambo.
Mtazame hapa chini Mrisho Gambo anavyoongea zaidi