Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA imekutana mchana huu kujadili juu ya hali ya kisiasa na mwenendo wa kesi inayowakabil viongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho ambao jana walisomewa mashtaka na kunyimwa dhamana. Viongozi waliokamatwa na kuwekwa mahabusu ni Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Vicent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Bara, Visiwani, John Mnyika na Salum Mwalimu, Mbunge wa Tarime Mjini, Easter Matiko na Mwenyekiti wa chama hicho kanda ya nyasa, Peter Msigwa.
Video:Breaking News: CHADEMA Wakutana Kikao Cha Ghafla Kuwajadili Akina MBOWE
0
March 28, 2018
Tags