Madiwani katika jiji la Paris wametupilia mbali hoja ambayo ililenga kufunga biashara ambayo imekuwa ikihusisha watu kulipia kukaa na midoli ya mapenzi kwa saa moja.
Wateja hulipishwa €89 ($109; £78) kukaa na midoli hiyo iliyotengenezwa kwa madini ya silicone.
Madiwani wa chama cha Kikomunisti pamoja na watetezi wa haki za wanawake walikuwa wameliomba Baraza la Jiji la Paris ambalo huhusika katika kusimamia jiji hilo kujadili uwezekano wa kufunga biashara hiyo ambayo imekuwa ikifahamika kama Xdolls.
Wamekuwa wakisema biashara hiyo inadhalilisha wanawake na kimsingi ni kama danguro.
Ni haramu kumiliki au kuendesha biashara ya danguro nchini Ufaransa.
Lakini polisi walifika katika biashara hiyo kabla ya mkutano wa baraza hilo la jiji kufanyika na wakatangaza kwamba hakuna sheria zozote zilizokuwa zimevunjwa.
Katika taarifa ya pamoja, madiwani wa chama cha Kikomunisti Nicolas Bonnet Oulaldj na Hervé Bégué walisema wamesikitishwa sana na uamuzi wa baraza hilo.
"Biashara hiyo, ambayo ina midoli ya ukubwa sawa na binadamu na inakaribia sana umbo la binadamu, ndio uvumbuzi wa karibuni zaidi wa kujaribu kurejesha biashara ya madanguro," walisema.
Walieleza kuwa Xdolls ni "kilele cha kuharibiwa kabisa kwa uhusiano wa wanawake na wanaume".
Midoli ya mapenzi imekuwa ikipata umaarufu nchi mbalimbali. Doli kwa jina Harmony la kampuni ya RealDoll iliyoanzishwa na Matt McMullen katika eneo la San Marcos, California huweza kutembea na hata kuzungumza
Wamesema biashara hiyo inafanyia mzaha suala la kudhalilishwa kwa wanawake na mitandao ya biashara ya ukahaba na biashara husika ya ulanguzi wa binadamu.
Jumba hilo lilifunguliwa mapema mwaka huu na kujieleza kama "kituo cha michezo".
Wateja wengi huwa ni wanaume lakini wachumba pia hutembelea kituo hicho kwa pamoja, mmiliki wa kituo hicho Joachim Lousquy, ambaye zamani alimiliki maduka ya kuuza sigara, aliambia gazeti la Le Parisien.
Jumba hilo lina vyumba vitatu ambapo kila chumba kina doli la mapenzi la urefu wa 1m 45cm (futi 4 inchi 7) vya thamani ya euro elfu kadha.
Anwani ya jumba hilo huwekwa ikiwa siri kubwa na hata majirani huwa hawafahamu ni biashara ya aina gani hufanyika humo, anasema Lousguy.
Anasema midoli hiyo ni sawa na vifaa vingine vya kujitosheleza kimapenzi na haoni ni jinsi gani vinawadhalilisha wanawake.
Midoli ya mapenzi imekuwa ikipata umaarufu nchi mbalimbali. Doli kwa jina Harmony la kampuni ya RealDoll iliyoanzishwa na Matt McMullen katika eneo la San Marcos, California huweza kutembea na hata kuzungumza.
Nchini Kenya wiki kadha zilizopita, doli la mapenzi lililobandikwa jina Samantha lilizua pia mjadala mkali.