Wakili wa Mwanafunzi Abdul Nondo, anayeendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Afunguka Tena Kunyimwa Kuonana na Mteja Wake


Wakili wa Mwanafunzi Abdul Nondo, anayeendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa upelelezi kufuatia madai ya kutekwa, amesema mpaka sasa amefanya kila jitihada za kumuona mteja wake pasipo mafanikio.

"Kwa jitihada nilizofanya hadi sasa kumuona Abdul Nondo hazijazaa matunda. Hayupo vituo vikuu vyote, tukutane Mahakama Kuu kupitia Habeus Corpus watamleta wenyewe!" amesema Wakili Jebra Kambole.

Kauli hii ameitoa tena kufuatia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar, Lazaro Mambosasa kusema taarifa za Wakili huyo kuwa amezuiwa kumuona kijana huyo ni za uongo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad