Wambura Alia na Serikali Ukiukwaji wa Katiba

Wambura Alia na Serikali Ukiukwaji wa Katiba
Aliyekuwa makamu wa Rais wa shirikisho la soka nchini ambaye amefungiwa kutojihusisha na soka Michael Richard Wambura, ameiomba serikali kuingilia kati kitendo cha uteuzi wa Athumani Nyamlani kuwa makamu wa Rais wa TFF.


Wambura kupitia kwa mwanasheria wake Emmanuel Muga ameeleza kusikitishwa na vitendo vinavyofanywa na shirikisho hilo ambavyo havifuati katiba na ni ukiakwaji wa maadili wa chombo hicho cha Umma. Hivyo ameiomba serikali kuingilia ili kumaliza vitendo hivyo.

''Kamati Tendaji ya TFF imemteua Athumani Nyamlani kuwa Kaimu Makamu wa Rais, kinyume na Ibara ya 34 ya Katiba ya TFF ambayo haitoi mamlaka ya uteuzi kwa kamati Tendaji. Kwa uteuzi wa Bw. Nyamlani, TFF imevunja Ibara (34) a,b,c,d,e,f,g,h,i,j,k,l,m,n,o,p na q ya Katiba ya TFF toleo la 2015'', imeeleza taarifa ya Wambura.

Wakati huo pia Wambura amedai rufaa yake aliyokata kwa hati ya dharura, imecheleweshwa makusudi wakati wajumbe wote wa kamati ya rufaa wapo Dar es salaam huku akieleza kuwa kumekuwepo na ubadilishaji wa wajumbe wa kamati ya rufaa ya TFF bila kufuata kanuni.

Wambura ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali kwenye soka nchini ikiwemo ndani ya klabu ya Simba pamoja na chama cha soka mkoa wa Mara, amefungiwa maisha kutojihusisha na masuala ya soka.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad