Wananchi wamuomba Rais Magufuli kuingilia kati vitendo vya udhalilishaji vinavyofanya na Jeshi la polisi

Baadhi ya Wakazi wa Mtaa wa Kambarage Kata ya Buhalahala wilayani Geita katika Mkoa wa Geita wanaomba msaada kutoka kwa Rais Dk. John Magufuli kutokana na vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji vinavyofanywa na askari wa Jeshi la Polisi.

Wakizungumza katika mahojiano maalum na Muungwana Blog, walieleza Mwaka 2003, wananchi kushirikiana na wafadhili Mradi wa Plan walifanikisha kujenga kisima cha maji kwa ajili ya matumizi ya wakazi hao, ambapo kila Kaya ilichangia  kiasi cha shilingi 1000/= , jambo lililopelekea kupungua kwa kero ya maji.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kambarage Bw. Mfaume Habali, alifafanua kuwa uongozi wa Shule binafsi ya sekondari ya Waja uliunganisha mabomba kutoka shuleni hadi kisimani kwa ajili ya kuvuta bila kutoa taarifa kwenye uongozi wa serikali, jambo lililopelekea wananchi kugomea zoezi hilo.

Habali, alisema baada ya kuibuka mgogoro kati ya Shule ya Waja na wananchi taarifa zilimfikia Mkuu wa Wilaya na kuitisha ambapo aliitisha Mkutano wa Hadhara wakawa wamemaliza tofauti, lakini baada siku kadhaa wakandarasi wa mabomba walifika tena kuendeleza zoezi la kuvuta maji kutoka kisimani hapo, jambo lililopelekea wananchi kupiga mwano bila msaada.

"Mnamo Februari 22, mwaka huu polisi walivamia hapa mtaani na kuanza kuwapiga wananchi ovyo huku baadhi ya wakina mama walijikuta walinyanyaswa  kudhalilishwa, ambapo wengine waliacha miji yao na kukimbia kutafuta sehemu yenye usalama zaidi," alisema.

Mwenyekiti huyo alimpigia simu Mkuu wa Wilaya kumueleza juu ya vitendo vinavyofanywa na askari hao, ambapo mkuu wa wilaya alimpa jibu kwa njia ya ujumbe mfupi katika simu yake uliosomeka "Hakuna Hati Miliki ya Mitaa, nimewatuma mimi mwenyewe na yeyote atakayepinga hata kama ni wewe watakukamata. Agizo la Halmashauri haliwezi kupingwa na mtaa na wewe ni chanzo cha kuvuruga zoezi hilo".

Bw. Habali  aliwataja baadhi ya  wahanga katika tukio hilo, kwa wanawake ni Justa Fungameza na Fidelina Petro, baada ya kupigwa kuvulishwa nguo kisha kushikwa kifuani wakiwa hawana mavazi, huku kwa upande wa wanaume ni Msika Stima aliyepigwa na kitako cha bunduki kichwani kisha kuzimia, Reonard Lutama, Daud Stephano, Ephraim Odelo wao walipigwa na kushikiliwa kisha kupangiwa siku ya kuripoti mpaka Ijumaa iliopita waliambiwa warudi kituoni mpaka watakapowapatia sababu huku anaye washtaki hafiki na kutojulikana.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jeshi la polisi la kwetu lina mafunzo bado ya kizamani. Katika nchi nyingi polisi ni kama binadamu mwingine wa kawaida. Na si manyapala na wababe. Poisi wanahitaji mafunzo mapya.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad