Wanawake 527 Burundi Wameuzwa Uarabuni Kwa Kiasi Hiki cha Fedha


Ikiwa leo March 8, 2018 maadhimisho ya Siku wa Wanawake Duniani yakiendekea, kutoka nchini Burundi inaelezwa kuwa wanawake na wasichana zaidi ya 500 wa nchi hiyo wameuzwa katika biashara watu kwenda nchi za Uarabuni.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka ya shirika la kutetea haki za binadamu la ONLCT nchini Burundi, wanawake na wasichana hao wanapelekwa zaidi kwenye nchi za Oman, Saudi Arabia, Kuwait na Lebanon.

Uchunguzi ambao umefanywa na shirika hilo umebaini ya kuwa wanaojihusisha na biashara hiyo ya watu huwauza kwa hadi Dola za Marekani 1000 sawa na Shilingi za Tanzania Milioni 2.4 kwa kila mwanamke au msichana mmoja.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad