Wanawake nchini Poland
wameandamana kupinga serikali ya nchini hiyo kupitisha sheria mpya
ambayo itakataza moja kwa moja utoaji mimba wa aina yoyote ile.
Wanawake hao wakiwa wanaandamana pamoja na wanaharakati wa haki za
binadamu wameeleza kuwa kutoa mimba kukifanywa haramu kutahatarisha
maisha ya wanawake ambao maisha yao yanakuwa hatarini kutokana na kubeba
ujauzito.
Takribani mashirika yasiyo ya kiserikali 200
yamejiunga kwenye harakati hizo za kupinga serikali kukataza utoaji wa
mimba, kwa kuandika waraka wa rufaa kwa Bunge la nchi hiyo likisema
sheria hiyo itahatarisha maishaya wanawake.
Waraka huu pia umeungwa mkono na Ofisi ya Tume Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa.