Jeshi la Polisi limewaonya baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaoitumia vibaya kufanya uhalifu ikiwemo kuhamasisha 'maandamano haramu'
RPC Ahmed Msangi amesema "Kuna watu wanapeana vihabari vya kwenye mitandao ya kijamii wafanye uhalifu na uhalifu wenyewe ni wa kufanya maandamano au mkutano usiokuwa na taarifa na kiukweli imepigwa marufuku"
Aidha, RPC Msangi amewataka Polisi kufanya uchunguzi ili kuwabaini wanaoshinikiza hayo na kisha kuwahoji na kujua nia yao ya kutaka kufanya hivyo ni ipi
RPC Msangi ametoa onyo hilo wakati akizungumza na Polisi mbalimbali walipokuwa wakifanya mazoezi ya viungo katika uwanja wa Mabatini
Rais Magufuli, CDF Mabeyo, IGP Sirro na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ndio waliotangulia kutoa kauli hizi zinazoonyesha Vyombo vya Dola vimepania kupambana na waandamanaji (endapo itatokea) na kufuatiwa na Makamanda wa Polisi wa Mikoa kadhaa.