
Licha ya kutangazwa kutokea kwa ajali ya boti hiyo usiku wa Jumatatu hadi Jumamne nchini DRC jimboni Mayi -ndombe magharibi mwa mji mkuu wa Kinshasa,mbunge wa jimbo hilo ambae alitangaza taarifa hiyo alisema idadi aliyoitangaza awali hazikuwa za uhakika kwa kuwa taarifa alizopata hazikuwa za kweli. Lakini mara baada ya mbunge huyo kufika katika eneo la tukio alisema boti hiyo ilikuwa na abiria 121 na watu 108 wameokolewa huku watu 12 ndio wamepotea mpaka sasa na kifo cha mtoto moja wa miaka tano.
Aidha kuna ripoti kutoka kanisa la jimbo hilo wamesema kwamba watu kumi na tano ndio waliofariki ,Huku wahudumu wa afya wamethibitisha kupokea miili ishirini na tano na wakisema boti hiyo ilikwa na abiria wengi waliokuwa wakisafiri mjini Kinshasa.
Leo bado inasubiriwa ripoti kutoka msalaba mwekundu maana bado idadi kamili haijatajwa na imekuwa inatofautiana sana.
Ajali za boti zimekuwa zikiripotiwa karibu kila mwaka nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo kufuatana na ubovu wa boti na mashua na huku wakisafiri bila mavazi ya kujiokolea katika maji.