Tajiri huyo wa taxi anayejulikana kama Yaseen Abrahams siku za hivi karibuni ametangaza kuwa yeye na wenzake ambao wanahusika kwenye biashara hiyo watakuwa wanawapakia wazee wa miaka zaidi ya 70 bila kuwatoza gharama yoyote.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 25 aliandika tangazo hilo kwenye ukurasa wake wa Facebook akiwa kwenye mji mmoja karibu na Cape Town, jambo lililosababisha watu kumsifu kwa kuchukua hatua hiyo kuwasaidia wazee.