Wazee Kupanda Taxi Bure Afrika Kusini

Wazee Kupanda Taxi Bure Afrika KusiniStori Ninayokusogezea kutoka kwa Madiba yaani Afrika Kusini leo March 17, 2018 ni kwamba raia mmoja wa nchi hiyo ambaye anamiliki taxi kwaajili ya biashara akiwa wa wenzange wamezua hisia kali kwa watu baada ya kutangaza msaada kwa wazee.

Tajiri huyo wa taxi anayejulikana kama Yaseen Abrahams siku za hivi karibuni ametangaza kuwa yeye na wenzake ambao wanahusika kwenye biashara hiyo watakuwa wanawapakia wazee wa miaka zaidi ya 70 bila kuwatoza gharama yoyote.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 25 aliandika tangazo hilo kwenye ukurasa wake wa Facebook akiwa kwenye mji mmoja karibu na Cape Town, jambo lililosababisha watu kumsifu kwa kuchukua hatua hiyo kuwasaidia wazee.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad