Waziri Tizeba, Mpina Matatani kwa Kutohudhuria Mkutano wa Rais IKULU

Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina pamoja na Makatibu wao wameshindwa kuhudhuria mkutano wa 11 wa baraza la taifa la Biashara uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam na kuendeshwa na Rais Dkt Magufuli.

Katika mkutano huo Rais Magufuli aliwahitaji mawaziri hao ili waweze kutoa ufafanuzi kuhusu maswala ambayo yameibuliwa na wafanyabiashara, lakini mawaziri hao pamoja na Makatibu wao hawakufika licha ya kuwa walialikwa na kupaswa kuwepo kwenye mkutano huo.

Kufuatia kutokuwepo kwa viongozi hao, Rais Magufuli alimuuliza Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) kama waliweza kuwaalika mawaziri hao na ndipo Waziri Mkuu alipojibu kuwa walipata mualiko na walipaswa kuwepo kwenye mkutano huo ingawa hakukuwa na taarifa yoyote ya wao kutokuwepo wala kutuma wawakilishi wao.

"Kwa hiyo wa Kilimo na Mifugo mawaziri na Makatibu wakuu wote hawapo?............Wao sio wajumbe wa mkutano huu? Alihoji Rais Magufuli ndipo Mawaziri Mkuu aliibuka na kutoa majibu kwa Rais Magufuli.
"Mawaziri wote wanaoguswa na sekta za uwekezaji na "kusupport" uchumi wetu wa viwanda, kilimo ni "facilitater" (msimamizi) wa viwanda na Mifugo naye pia ni wa viwanda walikuw
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad