Jumla ya timu nane zilizofuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la shirikisho nchini leo zinatarajiwa kujua wapinzani wao katika hatua hiyo kufuatia droo itakayochezeshwa leo.
Shirikisho la soka nchini TFF kupitia kamati yake ya mashindano hayo limekuwa likitumia utaratibu wa kuchezesha droo kila inapoingia hatua mpya. Baada ya mechi za 16 bora kukamilika na timu 8 kupatikana leo mechi za kusaka timu nne za nusu fainali zitajulikana.
Mabingwa wa kwanza wa michuano hiyo klabu ya Yanga wamefuzu hatua hiyo huku mabingwa watetezi Simba wakiwa tayari wameshaondolewa katika hatua za awali na timu ya Green Worriors ambayo nayo iliondolewa na Singida United.
Timu zingine ambazo zimeingia kwenye nane bora ni Azam FC, Singida United, Mtibwa Sugar, Njombe Mji, Tanzania Prison, Stand United pamoja na timu moja kutoka ligi daraja la kwanza lakini imepanda kucheza ligi kuu msimu ujao JKT Tanzania.