MSHAMBULIAJI chipukizi wa Yanga, Yusuph Mhilu amesema, ana kila sababu ya kuipigania klabu yake ifanye vizuri tangu siku 'alipovutwa sikio' na kuambiwa aende akafanye kazi ya kuokoa jahazi lao lisizame.
Mhilu amesema, baada ya wachezaji wakubwa kama Wazimbabwe Donaldo Ngoma, Thaban
Kamusoko na Amiss Tambwe kuwa majeruhi kwa muda mrefu.
Yeye pamoja na wachezaji wengine chipukizi, walikalishwa chini na kuambiwa, timu inawategemea
wao na hivyo wanatakiwa kupambana na kuokoa jahazi la Yanga lisizame .
"Binafsi nina kila sababu ya kuipigania timu yangu ya Yanga baada ya wao kuniamini. Baada
ya kuona wachezaji wale wakubwa wamekuwa majeruhi wa muda mrefu na wao ndiyo walikuwa wanategemewa, sisi vijana tulikalishwa chini na kuambiwa ndiyo wa kwenda kuikoa Yanga na hivyo tukapambane,"anasema Mhilu.
Hata hivyo tangu kikosi hicho kianze kumtumia Mhilu na vijana wengine, mambo yamekuwa
mazuri ndani ya kikosi hicho ambapo sasa wako nafasi ya pili na pointi 46 sawa na za Simba
wanaoongoza, wakifuatiwa na Aazam FC yenye 44, Tanzania Prisons 26 na Singida iliyo ya tano 36.