Habari kutoka Mbagala Charambe leo March 6, 2018 ni kwamba zaidi ya vibanda 600 katika soko la Mkochela, vimeungua moto alfajiri ya leo na chanzo cha moto kinasadikiwa kuwa ni hitilafu ya umeme.
Afisa Habari wa Jeshi la Zima Moto Dar es Salaam Peter Mwambene ameeleza kuwa kwa mwaka huu hii ni mara ya pili, mwingine ulitokea mwezi February na sababu ya moto huu imekuwa ile ile kwa awamu zote mbili.
Mwambene pia ameeleza kuwa sababu ya moto huo kufanya uharibifu mkubwa ni kwamba vibanda vilikuwa vingi na ambavyo viko karibu karibu na ndani vilikuwa vina nguo ambazo zinachochea moto.
“Ni vizuri tukazingatia ujenzi wa kisasa wa mabanda ya biashara, mabanda ambayo yatapunguza athari endapo moto utatokea, lakini pia watu wawe na tahadhari ya vizimia moto vya awali, kwasababu havipo athari za moto zinakuwa kubwa zaidi.” – Peter Mwambene
Zaidi ya Vibanda 600 vya Wafanyabiashara Vyateketea kwa Moto Mbagala
0
March 06, 2018
Tags