Watu wameendelea kumiminika katika uwanja wa Orlando mjini Soweto Afrika Kusini kwa ajili ya maombolezo kwa mwanaharakati dhidi ya ubaguzi wa rangi
Winnie Madikizela-Mandela, aliyeaga dunia siku tisa zilizopita akiwa na miaka 81.
Mama Madikizela aliendelea na kampeni dhidi ya utawala wa mtu mweupe pale mume wake, Nelson Mandela alipokuwa gerezani, mwenyewe pia alikuwa kifungoni na kukutana na changamoto ya kuteswa na kufukuzwa.
Alizaliwa mwaka 1936 huko Eastern Cape wakati huo ulikuwa unajulikana kwa jina Transkei.
Image caption
Wakinamama wakiomboleza kifo cha Winnie Madikizela Mandela
Alikuwa akipata mafunzo kuhusu masuala ya ustawi wa jamii alipokutana na mumewe mtarajiwa mwaka 1950.Walipata watoto wawili.
Walikuwa wanandoa kwa miaka 38 ingawa kwa miongo takriban mitatu walikuwa wametengana kwa sababu ya kifungo kirefu.