Afungwa Miaka 32 Jela Kwa Kumpinga Nkuruzinza

Mahakama nchini Burundi imemhukumu mwanaharakati wa haki za binadamu, Germain Rukuki, kifungo cha miaka 32 jela baada ya kukutwa na hatia ya kushiriki katika maandamano dhidi ya Rais Pierre Nkurunzinza, wakati akiwania muhula wa tatu.


Rukuki anatuhumiwa kushiriki katika vuguvugu lililojaribu mapinduzi ya kijeshi na utekelezwaji wa mauaji ya askari polisi Mei 13, 2015, tarehe ambayo kundi la wanajeshi lilijaribu kumpindua Rais Nkurunzinza wakati akiwa nchini Tanzania.

Mwendesha mashtaka alimuongezea mashtaka mapya katika kesi hiyo ikiwemo mauaji, uharibifu wa mali ya umma, jaribio la kupindua utawala uliochaguliwa kidemokrasia makosa ambayo upande wa utetezi haukujulishwa
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad