Afya ya Aveva Yazidi Kuwa Mbaya Amelazwa Muhimbili........ Mahakama Yashindwa Kumsomea Maelezo ya Awali

Afya ya Aveva Yazidi Kuwa  Mbaya Amelazwa Muhimbili........Mahakama Yashindwa Kumsomea Maelezo ya Awali
Upande wa mashtaka umeshindwa kumsomea maelezo ya awali (Ph) Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ kwa sababu afya ya Aveva ni mbaya na amelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Hayo yameelezwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leonard Swai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Kisutu, Thomas Simba wakati shauri lilipoitishwa kwa ajili ya washtakiwa kusomewa (Ph).

Wakili Swai amedai kuwa afya ya mshtakiwa Aveva sio nzuri ‘very serious’ hivyo anaomba kesi hiyo iahirishwe hadi tarehe nyingine wakati wakisubiri afya ya Aveva iimarike.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Simba aliutaka upande wa mashtaka kuhakikisha unaandaa maelezo ya awali yawe tayari.

” Tunamuombea mungu afya yake iimarike ili siku tukianza kusikiliza, tuisikilize mfululizo, tumalize ili matokeo ya kesi yajulikane mapema.” amesema Hakimu Simba.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi April  25, 2018 ambapo washtakiwa hao watasomewa maelezo ya awali.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi na kutakatisha fedha dola za kimarekani 300,000.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad