Ajali ya Gari Yaua Wanafunzi Bukoba

Ajali ya Gari Yaua Wanafunzi Bukoba
Watoto wawili ambao ni wanafunzi wamefariki dunia leo kwa kugongwa na basi la Kampuni ya Frester basi lenye namba za usajili T720 DEV katika eneo la Katongo Luranda Bukoba mkoani Kagera na kisha gari hilo kupinduka.


Akiongea na www.eatv Kamanda wa Polisi mkoani humo Agustine Olomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, ambapo amesema watoto hao wawili walikuwa wanaelekea shule ndipo wakagongwa na basi hilo na kudai kuwa wamefanikiwa kumkamata dereva wa basi hilo.

Aidha Kamanda Olomi amesema kuwa majeruhi zaidi wa 20 ambao walikuwa kwenye basi hilo wamepelekwa hospitali kwa ajili ya kufanyiwa matibabu zaidi kutokana na majeraha waliyoyapata.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad