Arsenal Kuingia Mkataba Mnono na Kampuni ya Michezo ya Adida

Arsenal Kuingia Mkataba Mnono na Kampuni ya Michezo ya  Adida
Klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza imefikia hatua nzuri ya mazungumzo na kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas kuwa wadhamini wao wapya mkataba utakao gharimu thamani ya pauni milioni 40 kwa msimu.

Arsenal inatarajia kumaliza mkataba wake na kampuni ya vifaa vya michezo ya Puma mwishoni mwa msimu ujao ambapo The Gunners wameanza mchakato wa kutafuta kampuni nyingine mpya.

Kwenye makubaliano hayo kampuni ya adidas imeahidi kuongeza donge nono kama Arsenal itafanikiwa kufanya vizuri kwenye michuano ya Europa League.

Kampuni hiyo ya vifaa vya michezo inaihudumia klabu kubwa nyingine inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza kama Manchester United wenye mkataba wa pauni milioni 75 kwa mwaka wakati Chelsea akiwa na Nike na mkataba wao wa pauni milioni 60.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad