Askofu Cheyo Awaonya Watanzania " Fanyeni Kazi Njema Zinazompendeza Bwana"

Askofu Cheyo Awaonya Watanzania " Fanyeni Kazi Njema Zinazompendeza Bwana"Askofu Kiongozi wa  Moravian Tanzania jimbo la Kusini Magharibi Alinikisa Cheyo, amewaasa Watanzania kuacha kulalamika na badala yuake wajikite katika kufanya kazi njema inayompendeza Mungu.


Askofu Cheyo ametoa kauli hiyo katika ibada ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa Moravian Tanzania jimbo la kusini Magharibi ushirika wa Mbeya Mjini.

Askofu amesema ili  Watanzania waweze  kujiletea maendeleo yenye tija kufikia uchumi wa kati wanapaswa kuachana na mambo ya kisiasaili waweze  kufanya shughuli zao za kujiingizia kipato.

Askofu Cheyo pia ametumia fursa hiyo kuwaasa viongozi wake wengine wa dini nchini kutofautisha dini na siasa ili kujenga upendo miongoni mwa Watanzania ikiwa ni pamoja na kudumisha amani ya nchi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad