Dk. Shoo ambaye pia ni Askofu wa KKKT Dayosisi ya kaskazini, ameyasema hayo jana Jumapili Aprili 8, wakati akiongoza ibada katika Usharika wa Msaranga, mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Alisema katika dunia hii iliyojaa watu wenye midomo michafu, waliojaa viburi na unafiki mkubwa ambao hawaoni madhaifu yao ni vema Watanzania na Wakristo wakaungana katika kutoa maonyo dhidi ya watu hao kwa lengo la kuwafanya watu wote waishi kwa amani bila hofu.
“Katika dunia hii iliyojaa watu wa aina hiyo wenye kukata tama, wanaokataa maonyo, wasioona madhaifu yao na wanaokataa kutubu, Yesu anasema nimtume nani awapelekee ujumbe, kwa mantiki hiyo natamani kuona Wakristo watakatekeleza haya bila hofu.
“Kanisa linatamani kuona Watanzania wanaishi katika hali ya amani, upendo, mshikamano, maelewano pasipo kujali vyeo vyao wala itikadi zao za kisiana na ubaguzi wa kikabila na ukanda,” alisema.
Dk. Shoo alisema kumekuwa na watu wanaojinadi kwa maneno mazuri katika kuhubiri amani na mshikamano jambo ambalo halina uhalisia na kwamba Wakristo na Watanzania wana wajibu wa kusimama na kuhubiri amani na mshikamono wa kweli kwa vitendo.
“Katika nchi yetu kumekuwa na watu wanaojua kuyapamba maneno kweli kweli kisha wanasema wanahubiri amani ya Yesu mfufuka lakini maisha na mienendo yao iko kinyume kabisa na hilo hivyo wakati umefika Wakristo tuhubiri haki ya kweli, upendo na mshikamano,” alisema.
Kanisa lina Mchango Mkubwa sana wa kujenga Amani lakini halahala linapokengeuka, tumeyaona huko Rwanda, kwa kiasi kikubwa mauaji ya kimbari yalichagizwa moja kwa moja na makanisa na hususan viongozi wa makanisa hayo, wahanga wengi walifia ndani ya makanisa na walioongoza mipango ya mauaji hayo walikuwa ni viongozi hao wa makanisa ambao watu walikuwa na imani kubwa sana kwao, TUWE MAKINI NA VIONGOZI WA MAKANISA NA AGENDA ZILIZOFICHIKA.LULU (AMANI) TULIYONAYO TUITUNZE IKIPOTEA HATUTOIPATA TENA.
ReplyDelete